Picha za slide

Sunday, July 28, 2013

Atap Program

Mwana Atap Michael Mchome akifundisha  juu ya Ujasiliamali  na maana yake halisi mbele ya washiriki wa kanisa


Maana ya Ujasiriamali:

Uwezo na nia ya kukuza biashara, kuisimamia na kukabili hatari zote ili kutengeneza faida. Mfano mzuri wa uajasiriamali ni kuanzisha biashara mpya….Business Dictionary.com
Mtu ambaye badala ya kuajiriwa, anaendesha biashara yake na kukabili hatari zote na kupata matunda ya biashara yake. Mjasiriamali ni msimamizi na mbunifu wa wa biashara au wazo la kibiasharaInvestopedia…..2004
Mjasiriamali anaefanikiwa:
Mawasiliano na wajsiriamali wengine (Networking)
Daima jiamini (Self confidence)
Fanya matangazo ya biashara yako (advertisement)
Fanya Tafiti kutafuta biashara rahisi pia inayokubalika (Research)
Kubali kujitoa pia kupoteza (Risk taking)
Fanya tathmini ya biashara yako (Business Evaluation)
Heshimu biashara yako (Self Discipline)
Fanya Biashara kwa malengo (Business objective, goals)
Mfanye Mungu kuwa wa kwanza wakati wote (God is number one)

ATAP UBUNGO HILL

Wana Atap wa Kanisa la Waadventista Wa Sabato Ubungo Hill waliokwenda Dodoma kwenye mkutano wa Atap wakiimba  na kumtukuza Bwana siku ya Sabato mbele ya Washiriki wa Kanisa.Kulia ni Kiongozi wa Atap wa kanisa ndugu Elias Mabuba.

PF wa Kanisa la Ubungo

Watafuta njia  (PF)  wa Kanisa La Ubungo Hill sda church wakiwa kwenye picha ya pamoja kwenye viwanja vya kanisa tayari kwa safari ya kuelekea kundini  Kibo kwenye Program  maalum ya vijana.

Tuesday, July 2, 2013

Fanyeni hivi kwa ukumbusho wangu

Washiriki wakipokea divai  siku ya meza ya Bwana ndani ya Kanisa la Ubungo Hill
Shemasi wa zamu Yohana Kinoza akitoa huduma.

Sabato ya Meza ya Bwana

Huduma ya kutawadhana miguu  ikiendelea kabla ya kushiriki mkate na divai  29/6/2013
 (Siku ya Meza ya Bwana)

Monday, July 1, 2013

Meza ya Bwana

Sabato ya  Meza  ya Bwana  kanisa la Ubungo Hill ,ikiongozwa na wazee wa Kanisa kulia ni Mzee Nehemia Banabas na mzee Pius Lugomera wakishirikiana na mashemasi