Picha za slide

Saturday, August 24, 2013

Makambi Magomeni



Sabato ya Makambi kwenye viwanja vya kanisa la Waadventista Wasabato Magomeni 24/8/2013
Muhutubu mkuu  Pastor Clifford Goldstein  Editor, sabbath school Adult  lesson ,GC
Kushoto ni Mchungaji  Jonas Singu wa mtaa wa magomeni  na Dr U, Mpoki


Sunday, August 18, 2013

ECD Music Director


The ECD youth Chapleincy & music director  Pastor Magulilo Mwakalonge akiomba ombi la Mibaraka ya kazi ya uinjilisti ulio mpana sana wa usambazaji wa CD za kwaya  ya Kanisa zenye ujumbe wa Bwana  ni Mchungaji wangu vol 5 na Neema Kuu vol 6.

Mzee Kiongozi

Mzee Kiongozi wa Kanisa  Simon Nicolao akizindua rasmi Albamu  za Kwaya  ya Kanisa kwa kuzikabidhi mikononi mwa Mungu ili wengi wakaokolewe kupitia ujumbe uliopo ndani ya nyimbo hizo.

Uzinduzi Ubungo Choir

Kwaya ya Kanisa Ubungo Hill ikiwa mbele ya washiriki wa Kanisa kwa uzinduzi wa albumu zao mbili za Audio zilizobeba  majina ya Bwana ni mchungaji wangu vol 5 na Neema Kuu vol 6 siku ya sabato ya tarehe 17-8-2013

Sunday, August 11, 2013

Kiongozi wa Mawasiliano  Ubungo Hill ndugu E.Saguma akitoa maelezo  (Presentation)  juu ya ufanyaji kazi wa idara pamoja na taarifa rasmi juu ya warsha ya mawasiliano,alieleza kwamba:-

Warsha ya mawasiliano ya Divisheni ya Afrika Mashariki na kati,iliyoanza tarehe 6 Januari 2013 kwa usajili wa wajumbe imefunguliwa rasmi  tarehe 7 januari 2013 na kiongozi mkuu wa Tanzania Union Mchungaji Godwin Lekundayo akiambatana na katibu mkuu wa Tanzania Union Mchungaji David Fue, kiongozi wa mawasiliano kutoka Divisheni ya Afrika Mashariki Mchungaji Steve Bina, Mkuu wa conferensi ya Tanzania Mashariki Mchungaji Mark Warwa Marekana, Mkuu wa conferensi ya Nyanza kusini Mchungaji Joseph Bulengela, viongozi na wakuu wa mawasiliano wa nchi za Divisheni ya Afrika Mashariki na kati, viongozi wa mawasiliano confrensi na fildi za Tanzania,wakuu wa mawasiliano makanisani na wachungaji wa mitaa Tanzania.
Mada mbali mbali zitatolewa na wataalam mbalimbali na viongozi kutoka General confrensi;
1)John Becket – GC
2)Gundadoo - AWR
3) Professor E. Matiku - University of Africa
4) Dr. Rioba - University of Dar es Salaam
5) Pr. Steve Bina - ECD
6) Dr. Jim J. Yonazi - IFM
7) Engineer Kisaka - TRA
8) Dr. Hosea - PCCB


Pastor Mange

Pastor Suleiman Mange akihubiri katika sabato ya pekee sana ndani ya kanisa la waadventist Wa sabato Ubungo Hill.
Alilenga zaidi kwenye hubiri la kaya na familia kwamba ndio msingi wa mwanadamu, Mwanzo2:18
Alisisitiza upendo kwa wana ndoa na kwa kanisa  kiujumla ,ili nuru yetu iangaze kwa mataifa.
Vijana waliaswa kuwa na mipango madhubuti katika kutafuta wenza pindi umri unapofikia ,kwani ndio mpango wa Mungu ya kwamba kuwa na mtu wa kufanana nae.