Picha za slide

Sunday, April 20, 2014

Sasa Nazindua Rasmi

 Vice President wa Kanisa La Waadventista Wasabato  Pr Benjamin Shoun  ambaye pia Kiongozi wa Radio Ya  Wasabato Ulimwenguni (AWR), akibonyeza kitufe kuashiria kuzinduliwa rasmi kwa  MorningstarTV  kwenye viwanja vya SabaSaba ukumbi wa P.T.A. jijini Dar es Salaam Tanzania, akishuhudiwa na viongozi mbalimbali akiwemo pia  Mkurugenzi wa Mawasiliano  Pr Mika wa pili kulia


Uzinduzi Morningstar TV SabaSaba

Viongozi wa Kanisa la Waadventista Wasabato  kutoka kushoto ni Pr Bina anayefuata ni   President wa Division ya Africa Mashariki na Kati Pr. Blasius Ruguri  na Pr, Brad Thorp, Hope Channel president
 na mkewe  



Ubungo Hill Choir

 Kwaya ya Waadventista Wasabato Ubungo Hill wakiwa tayari kupanda jukwaani kwa ajili ya kumsifu Mungu katika kipindi cha Ibada Kuu kabla ya Muhutubu  wa Ibada kuu kusimama kwa ajili ya somo  maalumu ndani ya viwanja vya PTA Siku ya Sabato ya ufunguzi wa Morningstar Tv 19/4/2014
Ubungo Hill Choir wakiimba wimbo Maalum kabla ya Muhubiri Pr Benjamin Schoun kusimama na Kunena na wana na Binti za Mungu katika Viwanja vya Sabasaba ukumbi wa P.T.A


Temeke SDA Choir


 Kwaya ya Waadventista Wasabato Temeke wakimsifu Mungu Siku ya Uzinduzi Wa television ya Morningstar kwenye viwanja vya Sabasaba ukumbi wa P.T.A


Sunday, April 13, 2014

Imani Yenu Iko Wapi ?

Sabato ya pekee ndani ya Kanisa  la Waadventista Wa sabato Ubungo Hill mgeni kutoka East Centra Africa Division Pr Alain Coralie akihubiri siku ya sabato, akiwa na mfasiri Kushoto  ndugu Isack Nikolao.
Imani yenu iko wapi? Ni maneno aliyokuwa akisisitiza juu ya imani ndani yetu hasa kwa kila mshiriki kujitafakari imani yake iko kiasi gani kwa Mungu wetu .
Somo lilienga kitabu cha Luka 8:22-25 wakati ule Yesu alipokuwa chomboni  akivuka ngambo na wanafunzi wake .Mara tufani kubwa ikashuka juu ya ziwa,chombo kikaanza kujaa maji wakawa katika hatari.