Picha za slide

Tuesday, January 21, 2014

Msitikisike Kiimani

Mchungaji wa Mtaa wa Ubungo  Michael Zacharia Twakaniki  pamoja  na familia yake wakiimba wimbo  maalumu  wenye maneno yanayosema ndugu zangu msitikisike kiimani mkazidi kutenda kazi ya Bwana wetu Yesu siku zote.Kesheni simameni imara katika imani.Hayo ni maneno ya wimbo huu ulioimbwa na familia ya mchungaji  wakati akiagana na washiriki wa Kanisa la Ubungo hill ,kwa sasa mchungaji anaelekea kuchunga mtaa mwingine Dodoma .Wa pili kutoka kulia ni mke wa mchungaji .

Siku kumi za Maombi

Mchungaji wa Mtaa wa Ubungo Michael   Twakaniki   akiomba kwa unyenyekevu  siku ya sabato ya kuhitimisha siku kumi za kufunga na kuomba kwa kuungana na makanisa yote duniani katika siku hizo kumi za maombi  ndani ya kanisa la Waadventista Wa sabato Ubungo Hill.