Picha za slide

Tuesday, March 11, 2014

President Southern Tanzania Union.

Pr Magulilo Mwakalonge ,President wa Southern Tanzania Union akihubiri siku ya Sabato maalumu ya Muziki wa Kuabudu ndani ya Kanisa La Waadventista Wa sabato Ubungo Hill .Alizungumzia namna ambavyo tunapaswa kumuabudu Mungu wetu katika kicho na Kweli.Hata nyimbo zetu ziwe za kumtukuza Mungu  na kumwinua.Mungu ni Roho, nao wamwabuduo yeye imewapasa kumwabudu katika Roho na kweli.Alitoa mfano wa kisa cha Mwanamke Msamalia ambacho kinapatikana katika kitabu cha Yohana 4

Muziki Day

Pr Magulilo Mwakalonge ,President wa Southern Tanzania Union na mkewe wakisalimia washiriki wa Kanisa La Ubungo Hill ,waliokaa  ni Mzee kiongozi wa Kanisa Pius Lugomela na Mzee Jubily Msagasa

Muziki Day

Kanan Brothers wakimsifu Mungu  kwenye uimbaji siku ya sabato Maalumu ya Muziki wa Kuabudu.

AMO  hawakuwa nyuma kwenye Sabato Maalumu  ya Muziki wa Kuabudu tarehe 9/3/2014 ndani ya Kanisa La Waadventista Wa sabato Ubungo Hill

Muziki wa Kuabudu

Kwaya ya Kanisa la Waadventista Wa sabato Ubungo Hill wakiimba kwenye Sabato maalumu ya Muziki wa Kuabudu .Ilikuwa Sabato ya  pekee sana kwani kulikuwa na ugeni mkubwa wa Presidenti  wetu  Southern Tanzania Union
 Pr Magullilo Mwakalonge  pamoja na mke wake.