Picha za slide

Monday, November 10, 2014

Mazishi Ya Mmisionari.

 Mchungaji Mussa Mitekero akiwa Amelibeba Jeneza La Marehemu Mrs James Twing ambaye alifariki  30july 2014 huko USA Marekani alisafirishwa na kuzikwa huko Morogoro Misufini.Mazishi yaliendeshwa na Pr David Fue.Mwili wake ulizikwa karibu na Marehemu Mumewe aliyefariki kwa ajali ya ndege 1972  Tanzania.

Monday, November 3, 2014

Uchangiaji MorningStarTv

Mchungaji Christopher Ungani ambaye ni Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Eastern Tanzania Conference,akihubiri kwenye Sabato maalumu ya uchangiaji wa Television ya MorningStar 1november2014,akiongozana na Amani Mwakalindile (Mkuu wa Mawasiliano Ubungo Hill) wa kwanza kulia na Samson Kamanga(Mkuu wa Mitambo). kwenye kanisa la Waadventista wasabato Ubungo Hill. Pastor  alijikita zaidi kwenye kitabu cha Yohana  na lile fungu linalosema; Basi Yesu alipokwisha kuipokea ile siki,alisema imekwisha,akainama kichwa, akaisalimu roho yake.
(Yohana 19:30)'TETELESTAI'