Picha za slide

Sunday, July 5, 2015

Kutoka San Antonio

Moja kwa moja Yaliyojili kwenye mkutano Mkuu wa General Conference huko San Antonio




San Antonio 2015 Safu GC



Siku ya Sabato viongozi wa ngazi ya juu ya kanisa pamoja na wake zao wakiwa mbele ya wajumbe wa mkutano mkuu wa kanisa.

Saturday, July 4, 2015

MIAKA MITANO TENA

Kwa mara nyingine tena Wajumbe wa Mkutano Mkuu Wa Waadventista Wasabato jana tarehe 2  kwa kauli moja Wamempitisha tena kwa muhula wa pili Ted N.C Wilson kuwa President wa Kanisa la Wasabato Ulimwenguni .Ushindi huu ni wa zaidi ya asilimia 90

Friday, July 3, 2015

Mkutano Mkuu Wa Kanisa


 Technolojia Hii ya kutumia kifaa Maalumu Huenda ikatumika na Wajumbe wa Mkutano Mkuu wa Waadventista Wasabato Ulimwenguni katika kupiga kura badara ya mfumo wa zamani wa kuandika au kutumia kadi kadi.Chini ni picha  za matukio za siku ya kwanza ya mkutano katika Mji wa San Antonio (GC SESSION 2015 2-11 JULY)


ARISE !SHINE !JESUS IS COMING


 Wajumbe mbalimbali wakiwasili tayari kwa mkutano .San Antonio



Friday, June 26, 2015

ARISE ! SHINE ! JESUS IS COMING!

Ondoka uangaze kwa kuwa nuru yako imekuja, na Utukufu wa Bwana Umekuzukia.
(Isaya 60:1-3)Wito Mkuu wa mkutano. Juu ni  Mwonekano wa upande mmojawapo wa eneo ambalo mkutano   Mkuu wa 60 General conference utakaofanyika San Antonio Convetion Center kuanzia tarehe 2-11 July 2015
Mandhali ya  eneo mojawapo kwa muonekano wa hotel ya Henry B Gonzalez Convertion center ambapo mkutuno Mkuu wa Kanisa la Wasabato utafanyika huko San Antonio 2015 kuazia 2-11 July

TAIN-Tanzania Adventist Internet Network

 Pastor Dr Lekundayo akimkabidhi Tuzo mmoja wa washiriki wa semina ya Mawasiliano Pr Mika kwenye mkutano mkubwa wa wana mawasiliano uliofanyika mjini Arusha 21 -25 june 2015
 Pr Mika akiwa katika zamu yake siku ya semina
Pr Bina mkuu wa Mawasiliano akimkabidhi Tuzo Mwenyekiti wa comference ya Kaskazin mwa Tanzania Dr Lwekundayo katika semina ya mawasiliano iliyofana TAIN katika kanisa la Waadventista wasabato jijini Arusha

Sunday, March 15, 2015

Siku Ya Wanawake ULimwenguni

Juu kushoto ni   Mama Judith Nikolao akiwa Muhutubu mkuu siku ya Wanawake katika Kanisa La waadventista Wasabato Ubungo Hill iliyofanyika tarehe 14march 2015.
Tazama matukio ya sabato ya Wanawake hapa chini.

Juu kulia ni Mama Joyce Chilagwire na Mama Agness Chezue kwa pamoja wakiwa na Muhutubu Mkuu.

Tuesday, February 10, 2015

Pastor Tedy Wilson

Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dr Jakaya Mrisho Kikwete alipowakaribisha Viongozi wa kanisa la Waadventista wa Sabato Ikulu jijini Dar es Salaam na kuwa na mazungumzo  ya pamoja. Pichani kushoto ni
 Pr Blasious Ruguri  na mkewe, na Pysical therapist Nancy Louise Vollmer mke wa Pr Tedy wilson

Sherehe za Utume (Extravaganza)Dar es salaam

 Siku ya sabato ya tarehe 7 Feb 2015 Pastor Tedy N.C. Wilson katikati na Mtafsiri wake Pr Mika picha juu ,wakiwasalimu maelfu ya washiriki waliofika katika uwanja mkuu wa Taifa


Saturday, February 7, 2015

Mkutano Mkuu wa UTume (Extravaganza)

Siku  ya sherehe za Ufunguzi wa mkutano mkuu   wa Extravaganza ,kiongozi wa Kanisa La Wasabato Ulimwenguni Pr ted N. C Wilson akiwasili kwenye uwanja Mkuu wa Taifa siku ya ijumaa
 6 feb 2015.Kutoka kushoto ni Pastor G.K Lekundayo,Elizabeth  Ruguli,Pr Blasious Ruguri na
 Pr Maggulilo Mwakalonge.



 Vijana wa Pathfinder wakipiga gwaride maalum mbele ya kiongozi wa Kanisa la Waadventista Wa sabato Ulimwenguni, wakimkaribisha kabla ya kuingia kwenye vyumba maalumu tayari kusaini kitabu cha wageni rasmi.

Wednesday, January 28, 2015

Siku ya kugawa Conference


Siku maalumu ya mkutano mkuu wa kugawa konferensi  yetu na kuzaliwa konferensi mbili
(SEC) na( ECT) ni Pr Brasious  Ruguli akikagua Gwaride
Viongozi walioteuliwa kwa mkutano wa january 2015
South Eastern Conference


Mwenyekiti: Mch. Mark Walwa Malekana
Katibu: Hebert Nziku
Mhazini: Yusuph Zege
Mkurugenzi wa Huduma: Mch Toto Kusaga
Vijana: Wilfred Mafwimbo
Elimu na Mawasiliano: Abrahamu Youze
Afya na Familia: Mwaibasa Whatson
Huduma za wanawake: Bernais Luuha