Sunday, September 23, 2012
WAATHIRIKA WA MOTO IKIZU WAPEWA MSAADA
Wanafunzi 100
wa Ikizu High School walioathirika kwa kupoteza mali zao kwenye ajali ya moto
uliochoma mabweni mawili wamepewa msaada na shirika la msaada la Kanisa la
Wa-adventista Wasabato (ADRA). Msaada huo uliotoka makao makuu ya kanisa la
Wa-Adventista Wasabato, Njiro, Arusha, na kukabidhiwa kwa mkuu wa wilaya ya
Bunda ndugu Joshua Mirumbe na mwenyekiti wa Konferensi ya Mara Mch. Daudi
Makoye.
Katika hafla
hiyo fupi, Mchungaji Makoye aliwashukuru wanafunzi, waalimu na wafanyakazi wa
jumuia ya Ikizu kwa kuonesha ukomavu mkubwa na kuwa watulivu na kue- ndelea na
masomo wakati tatizo lililowapata likishughulikiwa.
Wanafunafunzi
walionyesha furaha na kushangilia. Viongozi mbali mbali wa serikali
walioandamana na mkuu wa wilaya waliwahimiza wanafunzi kusoma kwa bidii ili
wachukue nafasi za mbalimbali taifani. Kwani hata mkuu wa wilaya mwenyewe
aliwatia moyo kwamba alisoma katika shule ya Ikizu. Alisema, shule ya Ikizu ni
kongwe na imetoa viongozi wengi hata katika ngazi ya taifa.
Mwalimu Masasi anayekaimu ukuu wa
shule alishukuru sana kanisa na uongozi wa serikali kwa kuonyesha moyo wa kujali
shule Ikizu na maswala ya jamii.
Friday, September 21, 2012
SATELLITE DATES CHANGES-Breaking News
I
have been informed this morning by Pr. Steve Bina, who is the ECD
Satellite Cordinator, that the Kampala Net Event (satellite evangelism)
of 2012 will now be uplinkeon from 29.09.2012 to 15.10.2012 instead of
the previous dates (22.09.2012 - 06.10.2012) due to unavoidable
technical reasons. We apologize for any inconvenience caused.
We are making announcement over Morning Star Radio regarding these
changes. However I appeal to all of us to cooperate in passing this
message to our downlink sites as fast as possible.
...
Kind Regards,
Pr Musa Mika
TU - Satellite Coordinator
Kind Regards,
Pr Musa Mika
TU - Satellite Coordinator
Wednesday, September 19, 2012
UFUNGUZI WA MKUTANO KANISA LA WASABATO USHINDI (WATERFRONT HALL)
WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Rais (Uhusiano na Uratibu)
Stephen Wassira ndie aliyekua mgeni rasmi siku hiyo ya ufunguzi akiwa na
mwenyeji wake Askofu wa kanisa wa Wasabato Tanzania Mchungaji Dk Godwin
Lekundayo.
Mh Steven Wassira alikagua gwaride ambalo lilikua
likiendeshwa na wanafunzi wa Herritage.
Mkutano huo bado unaendelea (Waterfront hall)
Friday, September 14, 2012
SATELLITE YAZINDULIWA KAMPALA UGANDA NA MHUTUBU Pr RUGURI
Wednesday, September 12, 2012
Team to probe Ikizu school fire
Authorities in Bunda district, Mara region
have formed a team of seven people to investigate the cause of a fire
that gutted down two dormitories at Ikizu secondary school.
Bunda District Commissioner, Joshua Mirumbe,
said the probe team will work under the district security committee. He
said there are rumors that the fire was an act of malice and not an
electrical fault as reported earlier by the school administration.
“The fire incident is suspected to be an act of
sabotage… I want the probe team to look into the matter thoroughly,” he
said.
Mirumbe said the team working with officials from
the fire brigade department, is expected to complete its task within
five days. He said the team is led by District Criminal Investigation
Officer who is the chairman while other members will come from the
police force, intelligence unit, village leaders and the school owner.
Mirumbe said the terms of reference include
identifying the cause of the fire and making recommendations on how to
avoid such an occurrence in future.
The incident occurred at around 9pm over the
weekend. It was preceded by a huge blast before the fire spread quickly
and burning down two dormitories with all the students' belongings.
Earlier, the Ikizu Secondary School Headmaster
Emmanuel Masasi said the fire was caused by an electrical fault. He said
the dormitories which were burnt down were used by100 Form One, Two and
Three students.
He said the fire started when students were
attending a preparatory session in the classrooms.
“No one was injured or killed during the incident,”
he said, adding that all students will remain at the school while the
administration communicate with their parents.
He called on Good Samaritans to volunteer support
to the students since they have lost all their personal belongings.
SOURCE:
THE GUARDIAN
Tuesday, September 11, 2012
UBUNGO HILL KWAYA''''WIMBO: "NEEMA IMENIOSHA DHAMBI"
Ubungo Hill Kwaya, Wimbo ni "NEEMA KWANGU BWANA KATOA IMENIFANYA MZIMA TENA" ni kipindi cha uimbaji na ushuhuda kila jumamosi asubuhi kuanzia 2.00-3.00!!
Monday, September 10, 2012
Wednesday, September 5, 2012
JK MGENI RASMI KONGAMANO LA WASABATO-TAR17 HADI 28 SEPT
Rais Jakaya Kikwete, anatarajia kuwa mgeni rasmi katika kongamano la maisha bora, lililoandaliwa na Kanisa la Waadiventista Wasabato kwa ajili ya kuwawezesha Watanzania kukabiliana na changamoto za maisha.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana, Mkurugenzi wa Habari na Mawasiliano wa Kanisa hilo, Mchungaji Musa Mika, alisema kanisa lake linatambua wajibu wake kwa jamii na Serikali katika kukabiliana na changamoto mbalimbali zinazoikabili nchi.
Alisema ili kukabiliana na changamoto hizo, kanisa limeandaa kongamano ambalo litachukua siku kumi kuanzia Septemba 17 hadi 28, mwaka huu jijini Dar es Salaam.
“Kanisa la Waadventista kama sehemu ya jamii, tunatambua changamoto zinazoikabili nchi yetu, ingawa jitihada kubwa zinafanywa na Serikali, mashirika ya dini pamoja na asasi mbalimbali.
“Leo kuna watoto wanaoitwa wa mtaani ama idadi ya wanaolelewa na mzazi mmoja inaongezeka kutokana na kuongezeka kwa talaka na ndoa zisizo na furaha na hali hii huathiri malezi ya watoto, elimu yao na maendeleo ya taifa kwa ujumla,” alisema Mika.
Alisema kongamano hilo la maisha bora limelenga katika kupanua uelewa ambapo mada mbalimbali zitajadiliwa, ikiwamo ukimwi, maadili kwa jamii, uhuru wa dini, ujasiriamali, mazingira, athari za imani za uchawi na namna ya kudumisha amani katika nchi yetu.
Saturday, September 1, 2012
MAKAMBI MTAA UBUNGO-2012
Kambi la mtaa wa Ubungo mwaka huu 2012 lilianza tarehe 18 mwezi wa 8 na kumalizika tarehe 25, likiendeshwa na Pr Orlando(Mjamaika) anayefanya kazi kama senior pastor huko nchini marekani. lilijumuisha makanisa ya Externa, Mabibo, Kibangu juu, Mpakani na wenyeji Ubungo hill. aliyenyosha kidole ndiye Pr Orlando na pembeni yake alikuwa mfasiri Pr Mbuti kusekwa.
Subscribe to:
Posts (Atom)