Wanafunzi 100
wa Ikizu High School walioathirika kwa kupoteza mali zao kwenye ajali ya moto
uliochoma mabweni mawili wamepewa msaada na shirika la msaada la Kanisa la
Wa-adventista Wasabato (ADRA). Msaada huo uliotoka makao makuu ya kanisa la
Wa-Adventista Wasabato, Njiro, Arusha, na kukabidhiwa kwa mkuu wa wilaya ya
Bunda ndugu Joshua Mirumbe na mwenyekiti wa Konferensi ya Mara Mch. Daudi
Makoye.
Katika hafla
hiyo fupi, Mchungaji Makoye aliwashukuru wanafunzi, waalimu na wafanyakazi wa
jumuia ya Ikizu kwa kuonesha ukomavu mkubwa na kuwa watulivu na kue- ndelea na
masomo wakati tatizo lililowapata likishughulikiwa.
Wanafunafunzi
walionyesha furaha na kushangilia. Viongozi mbali mbali wa serikali
walioandamana na mkuu wa wilaya waliwahimiza wanafunzi kusoma kwa bidii ili
wachukue nafasi za mbalimbali taifani. Kwani hata mkuu wa wilaya mwenyewe
aliwatia moyo kwamba alisoma katika shule ya Ikizu. Alisema, shule ya Ikizu ni
kongwe na imetoa viongozi wengi hata katika ngazi ya taifa.
Mwalimu Masasi anayekaimu ukuu wa
shule alishukuru sana kanisa na uongozi wa serikali kwa kuonyesha moyo wa kujali
shule Ikizu na maswala ya jamii.
No comments:
Post a Comment