Picha za slide

Sunday, June 16, 2013

Ibada Ubungo Hill

Mzee wa Kanisa Viva Ogada, akihubiri juu ya upendo wakati wa Ibada Kuu. Alisema

Moja ya mambo ya mwisho aliyoyakazia sana Kristo Yesu kabla ya kurudi mbinguni hata kuyatoa kama mojawapo ya amri zake ni Upendo. Yaani kumpenda Mungu kwa dhati  na Kupendana sisi kwa sisi.
Maagizo ya Bwana wetu YESU KRISTO kwa Kanisa ni kumpenda BWANA MUNGU wetu kwa dhati na utii. Alikazia fungu kutoka kitabu cha Marko 12:28-31

28Na mmojawapo wa waandishi akafika, akawasikia wakisemezana naye , akatambua  ya kuwa amewajibu vema , akamwuliza, katika amri zote ni ipi iliyo yakwanza? 
29 Yesu akamjibu, Ya kwanza ndiyo hii, Sikia Israeli ,BWANA MUNGU wetu ni BWANA mmoja; 
30 nawe mpende Bwana Mungu wako kwa moyo wako wote; na kwa roho yako yote na kwa akili zako zote, na kwa nguvu zako zote
.31 Na ya pili ndiyo hii, Mpende jirani kama nafsi yako. Hakuna amri nyingine iliyo kuu kuliko hizi”

No comments:

Post a Comment