Picha za slide

Monday, September 30, 2013

ACMS Arusha



Baadhi ya washiriki wa Semina kuhusu mfumo wa utunzaji wa taarifa za washiriki katika Kanisa la Waadventista Wa Sabato (ACMS) imemalizika jijini Arusha  tarehe 26/09/2013.
Semina hiyo iliyohudhuriwa na Makatibu wakuu pamoja na Wakuu wa Teknohama kutoka majimbo yote ya Kanisa la Waadventista Wa Sabato nchini Tanzania imekuwa na mafanikio makubwa kutokana na wahusika wote kuhudhuria kikamilifu. Akizungumza katika kuhitimisha semina hiyo, Msimamizi wa mfumo huo kutoka Makao Makuu ya Kanisa la Waadventista Wa Sabato Ulimwenguni Bi. Sherri Ingram-Hudgins, ametoa shukrani zake kwa Uongozi wa Tanzania Union pamoja na washiriki wote wa semina hiyo kwa ushirikiano waliouonyesha kwa muda wote wa semina.

Sunday, September 29, 2013

Shirika na Bwana

Mzee wa Kanisa John Mwakalonge kwa pamoja na Mzee kiongozi Simon nikolao kushoto wakiendesha huduma ya Meza ya Bwana
1Wakorintho 11:24
Naye akiisha kushukuru akaumega,akasema,huu ndio mwili wangu ulio kwa ajili yenu,fanyeni hivi kwa ukumbusho wangu
26: Maana kila mwulapo mkate huu na kukinywea kikombe hiki mwaitangaza mauti ya Bwana hata ajapo

Sabato ya Meza ya Bwana





Washiriki wa Kanisa la Ubungo Hill wakitawadhana miguu kabla ya kushiriki tendo takatifu la Meza ya Bwana

Tuesday, September 24, 2013

Siku ya Pathfinder Duniani

Kiongozi wa vijana watafuta njia (Pathfinder) wa kanisa la Ubungo Hill Mr Mapigano K Mapigano akihubiri katika siku ya watafuta njia Duniani.
Alihubiri juu ya habari ya kisa cha binti Yairo ambacho kinapatikana katika kitabu cha Luka 8
Ni namna gani mkono wa Yesu una nguvu ya kuokoa ,kuponya na kukuweka hai tena  pale tu utakapomtegemea.
Fungu la 41:  Na tazama mtu mmoja akaja jina lake Yairo naye ni mtu wa sinagogi akaanguka miguuni pa Yesu akamsihi aingie nyumbani kwake
42: Kwa kuwa binti yake yu katika kufa ……
51: Alipofika nyumbani hakuacha mtu kuingia pamoja naye ila Petro ,Yohana na Yakobo na babaye yule mtoto na mamaye
54: Akamshika mkono akapaza sauti akisema kijana inuka
55: Roho yake ikamrejea naye mara hiyo akasimama
Alisisitiza tumtegemee Yesu wakati wote.

Monday, September 2, 2013

Makambi Mtaa wa Ubungo



Makambi Mtaa wa UbungoKwaya ya Kanisa la Waadventista  wa Sabato Ubungo Hill wakiwa tayari kumsifu Mungu kwa njia ya uimbaji siku ya sabato 

BWANA AWAJUA WALIO WAKE

Pastor Japhet Joram Machage Muhutubu mkuu wa Makambi mtaa wa Ubungo akiwa na wahubiri wenza  kushoto ni Mchungaji Reuben Kingamkono kutoka mtaa wa Chuo kikuu na katikati ni Mchungaji Sadikiel Shehemba kutoka mtaa wa Ilala na Pastor Mjoge Gasogota  hayuko pichani kutoka Gairo.
Bwana awajua walio wake 2Timotheo 2:19
Lakini Msingi  wa Mungu ulio imara umesimama, wenye muhuri hii Bwana awajua walio wake. na tena kila alitajaye jina la Bwana na auache uovu.