Picha za slide

Monday, December 8, 2014

Sabato Ya Pekee!

Askofu Mkuu Wa Kanisa La Waadventista Wasabato Pr Mark Walwa Malekani akisisitiza jambo kwa Mchungaji wa Mtaa wa Ubungo  Pr Heri  Kuyenga Wakati wa Sabato  Maalumu  ya Uchangiaji wa ujenzi wa Kanisa kubwa la kisasa ambalo linatarajiwa kujengwa katika viwanja vya waadventista Wasabato Ubungo Hill.

Mti Wangu Mmoja


Siku maalumu ya uchangiaji wa MajengoMaarufu  kama Mti wangu Mmoja. Mzee wa Kanisa
 John Mwakalonge akielezea moja ya Picha ya mfano wa Kanisa linalotarajiwa kujengwa kwenye viwanja vya Kanisa La waadventista Wasabato Ubungo Hill.


Monday, December 1, 2014

Tukasa,Mabibo Hostel

 Mwinjilist L.Mwandambo akihitimisha effort iliyoandaliwa na wanafunzi wa chuo kikuu (TUKASA) kwenye viwanja vya Mabibo Hostel.Ilikuwa ni effort ya wiki mbili iliyomalizika siku ya Sabato ya
29November 2014.Kanisa la Ubungo Hill  kwa ujumla wake walishiri kwa namna ya pekee sana  siku hiyo.Ujumbe mkuu ulipatikana katika kitabu cha Waamuzi 16 juu ya Mnadhili wa Mungu Samson alivyo jiingiza kwenye mtego wa mwanamke Kahaba Delila.Effort hii iliongoa waumini wapya waliobatizwa (17) .

Monday, November 10, 2014

Mazishi Ya Mmisionari.

 Mchungaji Mussa Mitekero akiwa Amelibeba Jeneza La Marehemu Mrs James Twing ambaye alifariki  30july 2014 huko USA Marekani alisafirishwa na kuzikwa huko Morogoro Misufini.Mazishi yaliendeshwa na Pr David Fue.Mwili wake ulizikwa karibu na Marehemu Mumewe aliyefariki kwa ajali ya ndege 1972  Tanzania.

Monday, November 3, 2014

Uchangiaji MorningStarTv

Mchungaji Christopher Ungani ambaye ni Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Eastern Tanzania Conference,akihubiri kwenye Sabato maalumu ya uchangiaji wa Television ya MorningStar 1november2014,akiongozana na Amani Mwakalindile (Mkuu wa Mawasiliano Ubungo Hill) wa kwanza kulia na Samson Kamanga(Mkuu wa Mitambo). kwenye kanisa la Waadventista wasabato Ubungo Hill. Pastor  alijikita zaidi kwenye kitabu cha Yohana  na lile fungu linalosema; Basi Yesu alipokwisha kuipokea ile siki,alisema imekwisha,akainama kichwa, akaisalimu roho yake.
(Yohana 19:30)'TETELESTAI'

Monday, October 13, 2014

Adventures tupo!

Adventures wa Kanisa La waadventista Wasabato Ubungo Hill wakiwa tayari mbele ya Washiriki kwa Uimbaji siku ya PF

Pathfinder Day Ubungo Hill


 Pathfinder wa Kanisa La waadventista Wasabato Kipunguni wakiingia kwa Gwaride   kwenye  viwanja vya  kanisa  waadventista Wasabato Ubungo Hill siku ya PF iliyofanyika
11/oct/2014.Tazama Picha za matukio mbalimbali za siku hiyo




Wednesday, September 3, 2014

Tuvuke Jordan



Siku ya Sabato ya Makambi katika Viwanja vya Kanisa la Waadventista Wasabato Magomeni
Ni Pastor Grey  Clay Davis akihitimisha kwa neno la uzima  lililojengwa kwenye kitabu cha Yoshua 3&4 akiwa na  Mtafsiri wake  Mzee  Shani Mbibo.
 Greg Clay Davis is an engaging, captivating, passionate, highly experienced, well-traveled International Conference and Seminar Speaker, University Chaplain, Preacher and an Ordained Minister who speaks extensively on the Gospel, Family and Relationships, Youth Development, Personal Wellness and Entrepreneurship! He inspires corporate, social, and religious organizations across the globe

Makambi Magomeni Sda 2014


 Sabato ya Makambi Aug 30  katika viwanja vya Kanisa La waadventista Wasabato Magomeni.    Kutoka kushoto Mchungaji wa Kanisa la Magomeni  Pastor Safiel  Singo  Pr Mark W. Marekana  President of Eastern Tanzania Conference , Pr,Greg  Davis  na mtasfiri      Mzee wa  Kanisa Shani Kiswaga, Mchungaji  wa Mtaa wa Segerea Oscar Madatta Mashishanga  na  Mzee kiongozi wa  Kanisa la Magomeni Msafiri  Mbibo






Sunday, April 20, 2014

Sasa Nazindua Rasmi

 Vice President wa Kanisa La Waadventista Wasabato  Pr Benjamin Shoun  ambaye pia Kiongozi wa Radio Ya  Wasabato Ulimwenguni (AWR), akibonyeza kitufe kuashiria kuzinduliwa rasmi kwa  MorningstarTV  kwenye viwanja vya SabaSaba ukumbi wa P.T.A. jijini Dar es Salaam Tanzania, akishuhudiwa na viongozi mbalimbali akiwemo pia  Mkurugenzi wa Mawasiliano  Pr Mika wa pili kulia


Uzinduzi Morningstar TV SabaSaba

Viongozi wa Kanisa la Waadventista Wasabato  kutoka kushoto ni Pr Bina anayefuata ni   President wa Division ya Africa Mashariki na Kati Pr. Blasius Ruguri  na Pr, Brad Thorp, Hope Channel president
 na mkewe  



Ubungo Hill Choir

 Kwaya ya Waadventista Wasabato Ubungo Hill wakiwa tayari kupanda jukwaani kwa ajili ya kumsifu Mungu katika kipindi cha Ibada Kuu kabla ya Muhutubu  wa Ibada kuu kusimama kwa ajili ya somo  maalumu ndani ya viwanja vya PTA Siku ya Sabato ya ufunguzi wa Morningstar Tv 19/4/2014
Ubungo Hill Choir wakiimba wimbo Maalum kabla ya Muhubiri Pr Benjamin Schoun kusimama na Kunena na wana na Binti za Mungu katika Viwanja vya Sabasaba ukumbi wa P.T.A


Temeke SDA Choir


 Kwaya ya Waadventista Wasabato Temeke wakimsifu Mungu Siku ya Uzinduzi Wa television ya Morningstar kwenye viwanja vya Sabasaba ukumbi wa P.T.A


Sunday, April 13, 2014

Imani Yenu Iko Wapi ?

Sabato ya pekee ndani ya Kanisa  la Waadventista Wa sabato Ubungo Hill mgeni kutoka East Centra Africa Division Pr Alain Coralie akihubiri siku ya sabato, akiwa na mfasiri Kushoto  ndugu Isack Nikolao.
Imani yenu iko wapi? Ni maneno aliyokuwa akisisitiza juu ya imani ndani yetu hasa kwa kila mshiriki kujitafakari imani yake iko kiasi gani kwa Mungu wetu .
Somo lilienga kitabu cha Luka 8:22-25 wakati ule Yesu alipokuwa chomboni  akivuka ngambo na wanafunzi wake .Mara tufani kubwa ikashuka juu ya ziwa,chombo kikaanza kujaa maji wakawa katika hatari.

Tuesday, March 11, 2014

President Southern Tanzania Union.

Pr Magulilo Mwakalonge ,President wa Southern Tanzania Union akihubiri siku ya Sabato maalumu ya Muziki wa Kuabudu ndani ya Kanisa La Waadventista Wa sabato Ubungo Hill .Alizungumzia namna ambavyo tunapaswa kumuabudu Mungu wetu katika kicho na Kweli.Hata nyimbo zetu ziwe za kumtukuza Mungu  na kumwinua.Mungu ni Roho, nao wamwabuduo yeye imewapasa kumwabudu katika Roho na kweli.Alitoa mfano wa kisa cha Mwanamke Msamalia ambacho kinapatikana katika kitabu cha Yohana 4

Muziki Day

Pr Magulilo Mwakalonge ,President wa Southern Tanzania Union na mkewe wakisalimia washiriki wa Kanisa La Ubungo Hill ,waliokaa  ni Mzee kiongozi wa Kanisa Pius Lugomela na Mzee Jubily Msagasa

Muziki Day

Kanan Brothers wakimsifu Mungu  kwenye uimbaji siku ya sabato Maalumu ya Muziki wa Kuabudu.

AMO  hawakuwa nyuma kwenye Sabato Maalumu  ya Muziki wa Kuabudu tarehe 9/3/2014 ndani ya Kanisa La Waadventista Wa sabato Ubungo Hill

Muziki wa Kuabudu

Kwaya ya Kanisa la Waadventista Wa sabato Ubungo Hill wakiimba kwenye Sabato maalumu ya Muziki wa Kuabudu .Ilikuwa Sabato ya  pekee sana kwani kulikuwa na ugeni mkubwa wa Presidenti  wetu  Southern Tanzania Union
 Pr Magullilo Mwakalonge  pamoja na mke wake.

Tuesday, January 21, 2014

Msitikisike Kiimani

Mchungaji wa Mtaa wa Ubungo  Michael Zacharia Twakaniki  pamoja  na familia yake wakiimba wimbo  maalumu  wenye maneno yanayosema ndugu zangu msitikisike kiimani mkazidi kutenda kazi ya Bwana wetu Yesu siku zote.Kesheni simameni imara katika imani.Hayo ni maneno ya wimbo huu ulioimbwa na familia ya mchungaji  wakati akiagana na washiriki wa Kanisa la Ubungo hill ,kwa sasa mchungaji anaelekea kuchunga mtaa mwingine Dodoma .Wa pili kutoka kulia ni mke wa mchungaji .

Siku kumi za Maombi

Mchungaji wa Mtaa wa Ubungo Michael   Twakaniki   akiomba kwa unyenyekevu  siku ya sabato ya kuhitimisha siku kumi za kufunga na kuomba kwa kuungana na makanisa yote duniani katika siku hizo kumi za maombi  ndani ya kanisa la Waadventista Wa sabato Ubungo Hill.