Picha za slide

Friday, December 20, 2013

Safu Mpya Union Mpya

Safu ya Viongozi wa union mpya ya kusini  mwa Tanzania  katika picha ya pamoja katikati ni

Pr. Magulilo Mwakalonge - STUM President, kushoto ni

Mr. Jack Manongi - STUM Treasurer na kulia ni Pr. James Machage - STUM Executive Secretary. Uchaguzi wa viongozi  uliofanyika Nairobi  november 5/2013.



Sunday, November 10, 2013

Sabato ya Vijana

Mchungaji wa Mtaa wa Ubungo Pr Michael Twakaniki akihubiri siku ya sabato ya pamoja  ya  vijana wa mtaa  wa Ubungo
Alizungumzia zaidi ni namna gani imani yetu tumeijenga
mathayo 7 :24-27
Basi kila asikiaye haya maneno yangu na kuyafanya atafananishwa na mtu  mwenye akili,aliyejenga nyumba yake juu ya mwamba,mvua ikanyesha,mafuriko yakaja ,pepo zikavuma zikaipiga nyumba ile isianguke  kwa maana misingi yake imewekwa juu ya mwamba.
Alisisitiza tujenge imazi zetu juu ya mwamba na kamwe tusijenge juu ya mchanga fungu la 26

Mahafali

Kiongozi wa sauti ya unabii wa Kanisa la Waadventista Wa Sabato Ubungo hill Mama Eudora Minja akimkabidhi cheti mmoja wa wahitimu wa masomo ya gundua shule ya Msingi Ubungo Kisiwani 2013


Mahafali

Wanafunzi wa masomo ya Gundua na Sauti ya unabii kutoka shule ya Msingi Ubungo kisiwani wakiwa katika picha ya pamoja baada ya kuhitimu hatua ya 1 & 2 mwezi wa kumi 2013

Monday, September 30, 2013

ACMS Arusha



Baadhi ya washiriki wa Semina kuhusu mfumo wa utunzaji wa taarifa za washiriki katika Kanisa la Waadventista Wa Sabato (ACMS) imemalizika jijini Arusha  tarehe 26/09/2013.
Semina hiyo iliyohudhuriwa na Makatibu wakuu pamoja na Wakuu wa Teknohama kutoka majimbo yote ya Kanisa la Waadventista Wa Sabato nchini Tanzania imekuwa na mafanikio makubwa kutokana na wahusika wote kuhudhuria kikamilifu. Akizungumza katika kuhitimisha semina hiyo, Msimamizi wa mfumo huo kutoka Makao Makuu ya Kanisa la Waadventista Wa Sabato Ulimwenguni Bi. Sherri Ingram-Hudgins, ametoa shukrani zake kwa Uongozi wa Tanzania Union pamoja na washiriki wote wa semina hiyo kwa ushirikiano waliouonyesha kwa muda wote wa semina.

Sunday, September 29, 2013

Shirika na Bwana

Mzee wa Kanisa John Mwakalonge kwa pamoja na Mzee kiongozi Simon nikolao kushoto wakiendesha huduma ya Meza ya Bwana
1Wakorintho 11:24
Naye akiisha kushukuru akaumega,akasema,huu ndio mwili wangu ulio kwa ajili yenu,fanyeni hivi kwa ukumbusho wangu
26: Maana kila mwulapo mkate huu na kukinywea kikombe hiki mwaitangaza mauti ya Bwana hata ajapo

Sabato ya Meza ya Bwana





Washiriki wa Kanisa la Ubungo Hill wakitawadhana miguu kabla ya kushiriki tendo takatifu la Meza ya Bwana

Tuesday, September 24, 2013

Siku ya Pathfinder Duniani

Kiongozi wa vijana watafuta njia (Pathfinder) wa kanisa la Ubungo Hill Mr Mapigano K Mapigano akihubiri katika siku ya watafuta njia Duniani.
Alihubiri juu ya habari ya kisa cha binti Yairo ambacho kinapatikana katika kitabu cha Luka 8
Ni namna gani mkono wa Yesu una nguvu ya kuokoa ,kuponya na kukuweka hai tena  pale tu utakapomtegemea.
Fungu la 41:  Na tazama mtu mmoja akaja jina lake Yairo naye ni mtu wa sinagogi akaanguka miguuni pa Yesu akamsihi aingie nyumbani kwake
42: Kwa kuwa binti yake yu katika kufa ……
51: Alipofika nyumbani hakuacha mtu kuingia pamoja naye ila Petro ,Yohana na Yakobo na babaye yule mtoto na mamaye
54: Akamshika mkono akapaza sauti akisema kijana inuka
55: Roho yake ikamrejea naye mara hiyo akasimama
Alisisitiza tumtegemee Yesu wakati wote.