Picha za slide

Sunday, August 11, 2013

Kiongozi wa Mawasiliano  Ubungo Hill ndugu E.Saguma akitoa maelezo  (Presentation)  juu ya ufanyaji kazi wa idara pamoja na taarifa rasmi juu ya warsha ya mawasiliano,alieleza kwamba:-

Warsha ya mawasiliano ya Divisheni ya Afrika Mashariki na kati,iliyoanza tarehe 6 Januari 2013 kwa usajili wa wajumbe imefunguliwa rasmi  tarehe 7 januari 2013 na kiongozi mkuu wa Tanzania Union Mchungaji Godwin Lekundayo akiambatana na katibu mkuu wa Tanzania Union Mchungaji David Fue, kiongozi wa mawasiliano kutoka Divisheni ya Afrika Mashariki Mchungaji Steve Bina, Mkuu wa conferensi ya Tanzania Mashariki Mchungaji Mark Warwa Marekana, Mkuu wa conferensi ya Nyanza kusini Mchungaji Joseph Bulengela, viongozi na wakuu wa mawasiliano wa nchi za Divisheni ya Afrika Mashariki na kati, viongozi wa mawasiliano confrensi na fildi za Tanzania,wakuu wa mawasiliano makanisani na wachungaji wa mitaa Tanzania.
Mada mbali mbali zitatolewa na wataalam mbalimbali na viongozi kutoka General confrensi;
1)John Becket – GC
2)Gundadoo - AWR
3) Professor E. Matiku - University of Africa
4) Dr. Rioba - University of Dar es Salaam
5) Pr. Steve Bina - ECD
6) Dr. Jim J. Yonazi - IFM
7) Engineer Kisaka - TRA
8) Dr. Hosea - PCCB


No comments:

Post a Comment