Picha za slide

Wednesday, September 5, 2012

JK MGENI RASMI KONGAMANO LA WASABATO-TAR17 HADI 28 SEPT




Rais Jakaya Kikwete, anatarajia kuwa mgeni rasmi katika kongamano la maisha bora, lililoandaliwa na Kanisa la Waadiventista Wasabato kwa ajili ya kuwawezesha Watanzania kukabiliana na changamoto za maisha.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana, Mkurugenzi wa Habari na Mawasiliano wa Kanisa hilo, Mchungaji Musa Mika, alisema kanisa lake linatambua wajibu wake kwa jamii na Serikali katika kukabiliana na changamoto mbalimbali zinazoikabili nchi.

Alisema ili kukabiliana na changamoto hizo, kanisa limeandaa kongamano ambalo litachukua siku kumi kuanzia Septemba 17 hadi 28, mwaka huu jijini Dar es Salaam.

Kanisa la Waadventista kama sehemu ya jamii, tunatambua changamoto zinazoikabili nchi yetu, ingawa jitihada kubwa zinafanywa na Serikali, mashirika ya dini pamoja na asasi mbalimbali. 
 “Leo kuna watoto wanaoitwa wa mtaani ama idadi ya wanaolelewa na mzazi mmoja inaongezeka kutokana na kuongezeka kwa talaka na ndoa zisizo na furaha na hali hii huathiri malezi ya watoto, elimu yao na maendeleo ya taifa kwa ujumla,” alisema Mika.

Alisema kongamano hilo la maisha bora limelenga katika kupanua uelewa ambapo mada mbalimbali zitajadiliwa, ikiwamo ukimwi, maadili kwa jamii, uhuru wa dini, ujasiriamali, mazingira, athari za imani za uchawi na namna ya kudumisha amani katika nchi yetu.

No comments:

Post a Comment