Picha za slide

Tuesday, September 24, 2013

Siku ya Pathfinder Duniani

Kiongozi wa vijana watafuta njia (Pathfinder) wa kanisa la Ubungo Hill Mr Mapigano K Mapigano akihubiri katika siku ya watafuta njia Duniani.
Alihubiri juu ya habari ya kisa cha binti Yairo ambacho kinapatikana katika kitabu cha Luka 8
Ni namna gani mkono wa Yesu una nguvu ya kuokoa ,kuponya na kukuweka hai tena  pale tu utakapomtegemea.
Fungu la 41:  Na tazama mtu mmoja akaja jina lake Yairo naye ni mtu wa sinagogi akaanguka miguuni pa Yesu akamsihi aingie nyumbani kwake
42: Kwa kuwa binti yake yu katika kufa ……
51: Alipofika nyumbani hakuacha mtu kuingia pamoja naye ila Petro ,Yohana na Yakobo na babaye yule mtoto na mamaye
54: Akamshika mkono akapaza sauti akisema kijana inuka
55: Roho yake ikamrejea naye mara hiyo akasimama
Alisisitiza tumtegemee Yesu wakati wote.

No comments:

Post a Comment