Picha za slide

Monday, September 30, 2013

ACMS Arusha



Baadhi ya washiriki wa Semina kuhusu mfumo wa utunzaji wa taarifa za washiriki katika Kanisa la Waadventista Wa Sabato (ACMS) imemalizika jijini Arusha  tarehe 26/09/2013.
Semina hiyo iliyohudhuriwa na Makatibu wakuu pamoja na Wakuu wa Teknohama kutoka majimbo yote ya Kanisa la Waadventista Wa Sabato nchini Tanzania imekuwa na mafanikio makubwa kutokana na wahusika wote kuhudhuria kikamilifu. Akizungumza katika kuhitimisha semina hiyo, Msimamizi wa mfumo huo kutoka Makao Makuu ya Kanisa la Waadventista Wa Sabato Ulimwenguni Bi. Sherri Ingram-Hudgins, ametoa shukrani zake kwa Uongozi wa Tanzania Union pamoja na washiriki wote wa semina hiyo kwa ushirikiano waliouonyesha kwa muda wote wa semina.

No comments:

Post a Comment